NAFASI ZA KAZI
NAFASI: Muhudumu wa ofisi
KITUO CHA KAZI: Nyasubi Kahama
MUDA WA AJIRA: Mwaka mmoja.
ha foundation
Shirika la HA Foundation ni shirika lisilo la kiserikari lenye makao yake makuu nyasubi kahama , linatekeleza shughuli zake katika mkoa wa shinyanga wilayani kahama
MAELEZO KUHUSU MUHUDUMU WA OFISI.
- Kufanya usafi wa ofisi na maeneo yanayo zunguka
- kupokea wageni
- kufanya shughuli zingine atakazo pangiwa.
SIFA NA UZOEFU
UNAOTAKIWA:
- Awe binti au mwanamke Kijana kati ya umri wa miaka 15 had 24 anayekubalika katika jamii.
- Awe na Elimu siyo chini ya darasa la saba, mwenye uwezo wa kujieleza kwa ufasaha mbele ya wengine.
- Awe na uzoefu wa kufanya kazi
- Awe anajua kutumia koputa
- Awe na uwezo mzuri wa mawasiliano ya kuandika na kuzungumza katika lugha ya jamii husika pamoja na lugha ya taifa.
- Awe ana uwezo wa kuandika taarifa ya kazi
- Awe mkazi wa Nyasubi
- Awe na uwezo na utayari wa kufanya kazi katika muda tofauti kadri itakavyohitajika na pia awe binti au mwanamke kijana ambaye hatahitaji usimamizi wa karibu wa mtu mwingine
- Awe na sifa ya kuheshimu wengine na kutokuwa mbaguzi kwa namna yoyote.
Mtu yeyote ambaye anazo sifa zilizotajwa hapo juu awe huru
kuandika barua yake ya kuomba kazi hii na awasilishe barua ya maombi yake ya
kazi na muhtasari wa maelezo binafsi (CV).
Mwenyekiti
HA FOUNDATION
P.O Box 39
EMAIL: hafoundationtz@gmail.com
Wilaya ya Kahama
Simu na. 0768 088270
Wasilisha barua kwa mkono kwenye ofisi za shirika husika . Kwa msaada zaidi piga
simu tajwa hapo juu.
Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 5 Novemba, 2016


